Mbunge wa Momba David
Silinde amesema kwamba viwanda 366 vilivyokuwa vikifanya kazi nchini
mwaka 1984 vimekufa jambo linalosababisha vijana kukosa ajira nchini.
Mbunge ameyasema hayo wakati akitoa mchango wake wa mpango wa serikali wa mwaka 2016&2017 bungeni Dodoma
Baba wa Taifa Mwl. Julius
Nyerere alituachia viwanda 366 vikiwa vinafanya kazi kati ya hivyo
viwanda vya kubangua korosho vilikuwa 12,viwanda vikubwa vya nguo 12 na
vingine vingi lakini mpaka hivi sasa viwanda vya serikali vya kufanya
kazi hizo hakuna vilibinafsishwa na vingine vimebakia magofu.
Silinde ameongeza kuwa
kipindi hicho hicho shirika la ndege nchini lilikuwa na ndege
zinazofanya kazi 11 sasa hivi ndege ipo moja na serikali jitihada zake
kila mwaka hazionekani zikizaa matunda kunusuru hali hiyo.
Hata hivyo Mbunge huyo
amesema serikali bajeti yake ni ndogo kuliko hata bajeti ya kuendesha
taifa la Kenya na bado bajeti inategemea wahisani hivyo lazima serikali
haitaweza kukamilisha miradi iliyojiwekea.
No comments:
Post a Comment