Social Icons

Pages

Blogger templates

Wednesday, July 19, 2017

DK. KIGWANGALLA APIGA TAFU UJENZI WA JENGO LA MAKAO MAKUU YA CCM MKOA WA SONGWE


Na Mwandishi Wetu, Songwe
Mbunge wa Nzega Vijijini ambaye pia ni Mjumbe wa Halmashahuri Kuu ya Chama cha Mapinduzi (CCM) Taifa, Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla ambaye ni Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto, ametembelea kujionea maendeleo ya ujenzi wa Boma la jengo la ofisi za chama hicho kwa Mkoa wa Songwe huku akichangia kiasi cha shilingi Laki Tano.

Dk. Kigwangalla ambaye yupo kwenye ziara ya kikazi kwenye Mkoa huo mpya kwa ajili ya kukagua huduma za Afya ambapo alipata wasaha huo wa kutembelea jengo hilo na kueleza kuwa Serikali ya awamu ya tano ya CCM,  itaendelea kuboresha huduma  bora za afya kama Ilani inavyosema ambapo aliwataka wananchi kuendelea kumuunga  mkono Rais Magufuli katika juhudi zake mbalimbali za kulinda rasilimali za nchi.
“Rais wetu ameongeza bajeti ya dawa kwa kiasi kikubwa huku mpango wa kuokoa vifo vya akina Mama wajawazito na watoto wachanga tukilisimamia kwa nguvu zote.. Hii ni sera yetu na tuendelee kukiunga mkono chama chetu” alieleza Dk. Kigwangalla  na kisha alichangia kiasi cha Tsh. 500,000, kama mchango wake kwa ajili ya kuchangia maendeleo ya ujenzi huo wa jengo hilo la CCM Mkoa wa Songwe.
Mbali na kutembelea ofisi hizo za CCM, Dk. Kigwangalla alipata wasaha wakukagua Hospitali ya Vwawa na vituo mbalimbali vya Mkoa huo ikiwemo kituo cha Afya Mbuyuni na Iyula.
Wakati huo huo, Dk. Kigwangalla amemwagiza Mkurugenzi wa Wilaya ya Mbozi, Eliasey Ngowi kukamilisha  boma la chumba cha upasuaji linalojengwa katika kituo cha Afya Iyula na ujenzi wake ukamilike ndani ya miezi mine.
“Nakuagiza Mkurugenzi  boma ili la upasuaji likamilike ndani ya miezi mine. Na nitakuja hapa kulizindua mimi mwenyewe, ukae kwenye vikao vyenu huko na kushirikiana na Mbunge wa hapa, wananchi na hao wahisani muliowapata na mukamilishe haraka sana” alieleza Dk. Kigwangalla.
Aidha, alipongeza juhudi za watumishi wa sekta ya Afya kwa kuendelea kutoa huduma bora huku akimwagiza Mganga Mkuu wa Mkoa wa Songwe kuhakikisha anakamilisha mifumo ya maji ndani ya chumba cha upasuaji, Maabara na wodi ya Wazazi kwenye hospitali hiyo ya Vwawa.

No comments:

Post a Comment