Mkuu wa Mkoa wa Songwe Chiku Gallawa akizungumza na mafundi wanaojenga
katika kituo cha Afya Isansa Wilaya ya Mbozi, kituo hicho cha Afya
kimepokea shilingi milioni 500 kwa ajili ya upanuzi wa kituo hicho.
Grace Gwamagobe-Songwe.
Mkuu
wa Mkoa wa Songwe Chiku Gallawa amesema atahakikisha anasimamia kwa
ukaribu fedha zilizotolewa na serikali Mkoani hapa kwa ajili ya upanuzi
wa vituo vya afya ili zifanye kazi zaidi ya ile iliyopangwa awali
kutokana na kuongezeka kwa nguvu za wananchi.
Gallawa
ameyasema hayo mapema jana wakati wa ziara yake Wilaya ya Mbozi
alipokagua maendeleo ya upanuzi wa vituo vya afya vya Isansa
kilichopokea milioni 500 na kituo cha Afya cha Iyula Kilichopokea
milioni 400, kwa ajili ya ujenzi wa maabara, nyumba ya daktari, chumba
cha upasuaji, jengo la mama na mtoto na chumba cha kuhifadhia maiti.
“Fedha
hizi lazima zifanye kazi iliyopangwa vizuri na pia tuongeze kazi
nyingine ya ziada kutokana na kuwa tumepata nguvu ya wananchi lakini pia
mafundi wetu hawa tunaowatumia ni wazawa na wenyeji wa maeneo ya kwetu
kwahiyo gharama zao zitatupa unafuu ambao tunatakiwa kuutumia kuongeza
kazi nyingine”, amesema Gallawa.
Ameongeza
kuwa licha ya upanuzi wa vituo vya afya kuchelewa kuanza bado ana Imani
kuwa wataweza kumaliza ndani ya muda uliopangwa kutokana na uchapakazi
wa mafundi wazawa wa maeneo hayo.
Gallawa
amesema kukamilika upanuzi wa vituo hivyo vya afya kutavifanya vituo
hivyo vivutie na hata mgonjwa akifika apate matumaini ya kupona na sio
kukatishwa tamaa na hali mbovu ya mazingira.
“Tiba
ya kwanza ya mgonjwa akifika kituo cha afya akute mazingira yanavutia
na sio majengo mabovu na uchafu hivyo vitamfanya akate tamaa ya kupata
matibabu sahihi, tukimaliza ujenzi wa hayo majengo tutahakikisha
tunapaka rangi paa za majengo yote zifanane ili vituo vyetu vya afya
vivutie”, amefafanua Gallawa.
Aidha
Gallawa amemtaka Kaimu Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Mbozi
Lauteri Kanoni kuhakikisha anaweka mfumo wa maji safi katika vituo hivyo
hasa mfumo wa kuvuna maji ya mvua ili vituo vikikamilika maji yawepo
kwa ajili ya matumizi.
Naye
Mkazi wa kijiji cha Isansa Wilaya ya Mbozi Bi Stela Mkeya ameonyeshwa
kufurahishwa na upanuzi wa kituo cha Afya Isansa huku akieleza baadhi ya
kero walizokuwa wakizipata awali.
“Tunaishukuru
sana serikali ya Magufuli kwakweli wametusaidia, tulikuwa tunapata
shida kufuata huduma za upasuaji wa akina mama wajawazito huko hospitali
ya Wilaya iliyopo Vwawa lakini pia hapa kwenye kituo cha afya mzazi
akijifungua hata mazingira ya kwenda kujisafisha vizuri kama vile mabafu
yakiwa hayatoshi kabisa”, ameeleza Bi Mkeya.
Kwa
upande wao mafundi waliokabidhiwa kazi ya upanuzi wa vituo hivyo vya
Afya wameonyesha ari ya kufanya kazi hiyo kwa ufanisi na haraka huku
wakimuomba Mkuu wa Mkoa Chiku Gallawa awasaidie upatikanaji wa taa ili
waweze kufanya kazi mchana na usiku naye Mkuu wa Mkoa amekubaliana na
mapendekezo hayo.
No comments:
Post a Comment