Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za
Mitaa(TAMISEMI) Mhe George Simachawene akiongea na Waandishi wa Habari
(Hawapo Pichani) kuhusu kuanzishwa kwa Mkoa mpya waSongwe na Wilaya sita
mpya Picha na raymond M
(Na Raymond Mushumbusi-maelezo)
Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania Mhe.John Pombe Joseph Magufuli ameidhinisha
kuanzishwa kwa mkoa mpya wa Songwe na wilaya nyingine mpya nchini.
Akitoa tamko hilo
kwa niaba ya Rais Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na
Serikali za Mitaa(TAMISEMI) Mhe George Simachawene amesema kwa mujibu wa
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 imempa Mamlaka
Rais ya kugawa Nchi kwa kadri ambavyo atakapoona inafaa.
Mhe
George Simachawene amesema kutokana na mamlaka hayo aliyopewa Rais
jumla ya Wilaya sita na Mkoa mmoja wa Songwe umeanzishwa kwa mujibu wa
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 na Mkoa mpya wa
Songwe umeanzishwa kutoka Mkoa wa Mbeya.
Amezitaja Wilaya
mpya zilizoanzishwa kuwa ni Wilaya ya Songwe Mkoa wa Songwe,Wilaya ya
Ubungo Mkoa wa Dar es salaam, Wilaya ya Kibiti Mkoa wa Pwani, Wilaya ya
Kigamboni Dar es salaam, Wilaya ya Mlanyi Mkoa wa Morogoro na Wilaya ya
Tanganyika Mkoa wa Katavi.
“ Nichukue fursa
hii kuwaagiza Wakuu wa Mikoa wote ambao Wilaya mpya zimeanzishwa kufanya
maandalizi rasmi ili Mkoa na Wilaya hizo ziweze kuanza kufanya
kazi,aidha mkazo uwekwe kwenye upatikanaji wa Ofisi na huduma zote
muhimu kupatikana kwa urahisi katika Mkoa naWilaya hizo mpya” Alisema
Mhe Simbachawene.
No comments:
Post a Comment