Social Icons

Pages

Blogger templates

Monday, August 29, 2016

Polisi mkoani Songwe washutumiwa kumpiga na kumuua mkazi wa eneo hilo.


Jeshi la polisi mkoani Songwe limeingia kwenye dosari baada ya askari wa kituo cha Mlowo kudaiwa kumpiga na kumuuwa mwananchi mkazi wa eneo hilo, tukio lililotekelezwa 26 Aug 2016 majira ya saa nne usiku wakati marehemu akirejea nyumbani kwake.

ITV imeshuhudia umati mkubwa uliofurika nyumbani kwa marehem STANS KALINGA (42) mkazi wa Mlowo, anayedaiwa kuawa na jeshi la polisi kwa kosa la uzurulaji na uzembe, kama anavyoeleza kamanda wa jeshi la polisi Mkoa Songwe MATHIAS NYANGE.
Hapa wananchi wanaeleza hoja , kwa kuwa aliyeongoza doria hiyo ni mkuu wakituo cha polisi Mlowo, ni hatua zipi zitachukuliwa dhidi yake?
Kamanda wa polisi mkoa songwe Mathius Nyange, katika kujibu hoja zilizowasilishwa na wananchi hao, amesema kuwa  askali wote waliohusika watachukuliwa hatua kali za kisheria.
Marehemu  Stans Kalinga amefikwa na umauti katika hospitali ya vwawa alipopelekwa kutibiwa majeraha anayodaiwa kupigwa na askali polisi.
Chanzo ITV

No comments:

Post a Comment