Na
Lulu Mussa
Songwe
Wakazi
wa Wilaya ya Ileje Mkoani Songwe wamehamasishwa kutunza Vyanzo vya Maji kwakuwa
Maji hayana mmadala wa kitu chochote. Waziri wa Nchi mwenye dhamana ya
Usimamizi wa Masuala ya Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba ameyasema
hayo leo katika muendelezo wa ziara yake ya kukagua mazingira nchini.
Akiwa katika Kijiji cha Ibungu Wilayani Ileje,
Waziri Makamba alishuhudia uliochepushwaji wa Mto Kalembo kwa manufaa ya baadhi
ya mtu/watu, na haikuweza kufahamika mara moja muhusika. Aidha Waziri Makamba
amemuagiza Mkuu wa Wilaya ya Ileje Bw. Joseph Modest Mkude kuhakisha wanambaini
mtu/watu hao na kuwafisha katika vyombo vya Sheria.
Taarifa iliyotolewa na Mkuu wa wilaya ya Ileje ilisema kwamba
kumekuwa na uvamizi katika Vyanzo vya Maji na Serikikali imeendelea na juhudi
za kuwaondoa kwa kuwapatia maeneo mengine ila baadhi ya wananchi hao wamekuwa
wakikaidi. Hali hiyo haikumfurahisha Waziri Makamba na kuagizia kutumika
mamlaka ya Dola. "Hatuwezi kuruhusu watu kuharibu Vyanzo vya Maji na
kuwabembeleza watoke" Makamba alilisitiza.
Waziri Makamba amesema ni muhimu watu kutii Sheria na Mamlaka
zilizopo, ameagiza wakazi hao kupewa wiki mbili tu na baada ya hapo waondolewe
kwa nguvu kwani tayari maeneo mbadala kwa makazi yao yalisha ainishwa. Pia
Waziri Makamba ameahidi kutoa muongozo wa Sheria ndogondogo za Mazingira za
Vijiji na Vitongoji ili zitumike kama nyenzo za hifadhi ya Mazingira Nchini.
Katika hatua nyingine Waziri Makamba alitembelea Kijiji cha
Lubanda, Kata ya Lubanda na kufanya Mkutano wa hadhara na wananchi na
kuwasisitizia, kutokokata miti ovyo, kutochoma misitu na kuepuka uchepushaji wa
Vyanzo vya Maji ikiwemo mito na Mabonde.
Pia Waziri Makamba aliwashauri wakazi wa Lubanda kulima
kilimo cha Matuta ama makinga maji ili kuepuka mmomonyoko wa udongo katika
miinuko. Aidha Waziri Makamba ameunga mkono jitahada za wananchi wa Kata hiyo
za ujenzi wa Kituo cha afya kwa kuchangia bati Ishirini na nane (28). Waziri
Makamba anaendelea na ziara yake na leo amewasili katika Mkoa wa Rukwa.
No comments:
Post a Comment