POLISI katika Mkoa wa Songwe wamekamata kilogramu 455 za mbegu
zinazoaminika kuwa feki za mahindi katika msako mkali unaoendelea kwa
ushirikiano na Kampuni ya Mbegu ya Pana.
Kadhalika, watu watano wanashikiliwa na Polisi kutokana na
kujihusisha na biashara hiyo ya kuuza mbegu hizo na uchunguzi dhidi yao
unaendelea kufanyika.
Miongoni mwa maeneo ambayo msako umeendeshwa ni Mji Mdogo wa Mlowo
wilayani Mbozi ambako ndiko zimekamatwa mbegu hizo za mahindi.
Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Songwe, Mkuu wa
mkoa huo, Chiku Galawa amebainisha hayo alipozungumza na waandishi wa
habari ofisini kwake jana baada ya kukamatwa kwa mbegu hizo feki kuwa
serikali mkoani hapa imejipanga kuhakikisha wauzaji pembejeo feki wote
wanakamatwa na kuchukuliwa hatua za kisheria kwa kuwaumiza wakulima.
Hata hivyo, Galawa aliwataka wananchi kutoa ushirikiano mkubwa kwa
jeshi la polisi ili kuwafichua watu wanaojihusisha na biashara hiyo ili
wakamatwe na kufikishwa katika vyombo vya sheria kwani wanachangia
kudidimiza mapato ya mkulima kwa asilimia 80.
No comments:
Post a Comment