Na Beatrice Lyimo-MAELEZO
Umoja
wa Kilimo cha mbogamboga, matunda na nafaka umetoa wito kwa vijana
kutumia fursa zilizopo kwenye Sekta ya Kilimo na si kusubiri kuajiriwa.
Hayo
yamesemwa na Mwenyekiti wa Umoja huo Joseph
Kunguru wakati akizungumza na waandhishi wa habari kuhusu mradi kambi ya
kilimo ulioanzishwa na Umoja huo.
Mwenyekiti
huyo alisema kuwa wameandaa mradi huo kwa lengo la kuhamasisha vijana
kuona kilimo ni ajira na pia kilimo ni biashara.
“Tuna
wanachama 74 ambao wanatarajia kwenda kambini ambapo kati ya hao vijana
23 ni wahitimu wa vyuo vikuu, watapatiwa mashamba, mbegu, vitendea kazi
pamoja na chakula katika muda watakao kuwa huko ili kuwafanya waweze
kumudu katika shughuli za kilimo” alisema Bwa. Kunguru.
Aidha,
alisema kuwa umoja huo unaunga mkono jitihada za Serikali katika
kupambana na madawa ya kulevya kwa kuwachukua vijana ambao wameshapata
matibabu kujiunga na mradi huo ili kuweza kuwafanya wasirudi tena
vijiweni.
Akifafanua
zaidi Bwa. Kunguru alisema kuwa ili kuendesha umoja huo kiuchumi kila
mwanachama kwenye kila zao atachangia asilimia tano ya mapato kwenye
umoja kama fidia ya vifaa pamoja na mbegu walizopata kutoka kwenye umoja
huo.
Mbali na hayo, umoja huo umepanga kuanzisha ligi ya mpira wa miguu itakayojulikana kama Kilimo Kapu
kwa lengo la kuhamasisha vijana kujiunga kwa pamoja kama vikundi ili
kuweza kuwa na kambi za maendeleo ili kuweza kujikwamua kiuchumi na
kuinua pato la taifa.
MWISHO
No comments:
Post a Comment