Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akipata maelezo kutoka kwa Mwanachuo wa Chuo cha DIT,
Grolia Shoo kuhusu Mradi wa Ujenzi wa Nyumba za watumishi wa Halmashauri ya
Wilaya ya Momba zinazojengwa na Shirika la Taifa la Nyumba katika eneo la
Chitete wialyani Momba Julai 21, 2017. Gloria anafanya kazi kwa
muda akijifunza katika shirika hilo. Kushoto kwake ni mkewe Mary na
wapili kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Nyumba la Taifa, NHC,
Blandina Nyoni. (PICHA NA OFISI YA WAZIRI MKUU)
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akiweka jiwe la Msingi la ujenzi wa nyumba 20 za
watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Momba katika eneo la Chitete akiwa
katika ziara ya mkoa wa Songwe Julai 21, 2017. Wapili kulia ni mkewe Mary
na kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Chiku Galawa. Kulia kwa Waziri Mkuu
ni Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) linalojenga
nyumba hizo, Blandina Nyoni.
No comments:
Post a Comment