Social Icons

Pages

Blogger templates

Wednesday, October 4, 2017

WAZIRI APIGIA DEBE UTALII KUSINI

 WAZIRI wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Dk. Agustine Mahiga, amesema mikoa ya nyanda za juu kusini ina uwezo mkubwa wa kuboresha utalii kwa sababu ina rasilimali nyingi za maliasili.
Dk. Mahiga aliyasema hayo jana wakati akifunga maonyesho ya utalii yajulikanayo kama “karibu kusini” ambayo yalikuwa na kauli mbiu ya “utalii endelevu ni nguzo ya maendeleo ya viwanda.”
Maonyesho hayo yalifanyika mjini hapa ambapo yalikwenda sambamba na wiki ya utalii duniani.

Dk. Mahiga alisema dhana ya kukuza utalii kusini mwa Tanzania inatakiwa kwenda sambamba na dhana ya maendeleo ya viwanda ambavyo Tanzania imejizatiti kuvijenga kuelekea uchumi wa kati ifikapo 2025.

Alilitaka Shirika la Viwanda Vidogo Vidogo (Sido) kufanya kazi kwa kujituma ili wajasiriamali waliojitokeza wawe wafanyabiashara wakubwa na kuwainua wajasiriamali wadogo.

Hery Marere, mwakilishi wa wajasiriamali wa Sido kutoka Mkoa wa Njombe, aliiomba serikali kuwasaidia malighafi ambazo zinatumika kuzalisha bidhaa zao kutokana na kutopatikana nchini, hivyo kuwawia vigumu kuendelea kutengeneza bidhaa.

Pia aliiomba serikali ili Sido kwa kushirikiana na wajasiriamali wapewe kibali cha kuanzisha benki yao ili iwe rahisi kupata mikopo nafuu ili waweze kuendana na kasi ya uchumi wa kati na viwanda.

Chanzo:Nipashe

No comments:

Post a Comment